Cha Kutumaini Sina, Ila Damu yake Yesu (The Holy Drill)歌词由Mesh Kiviu Msanii演唱,出自专辑《Cha Kutumaini Sina, Ila Damu yake Yesu (The Holy Drill)》,下面是《Cha Kutumaini Sina, Ila Damu yake Yesu (The Holy Drill)》完整版歌词!
Cha Kutumaini Sina, Ila Damu yake Yesu (The Holy Drill)歌词完整版
Cha kutumaini sina
Ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha
Dhambi zangu kuziosha;
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Njia yangu iwe ndefu
Yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga
Nguvu zake ndiyo nanga.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Damu yake na sadaka
Nategemea daima,
Yote chini yakiisha,
Mwokozi atanitosha.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Nikiitwa hukumuni,
Rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake
Sina hofu mbele zake.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama